Mangasini Scanda "BIKO"

Actor/Director
Share:

Personal Info

  • Birth Name: Mangasini Scanda "BIKO"
  • Date of Birth: 24, Sep 1992
Social:

Biography

Mangasini Scanda almaarufu “Biko” kama wengi wanavyomfahamu kwenye sanaa ya Uigizaji, alizaliwa mnamo 24/9/1992 Mkoani Tabora akiwa ni mtoto wa tisa katika familiya ya watoto tisa,alihitimu elimu ya sekondari katika shule ya Minaki 2013, na baadae kujiunga katika chuo cha Tumaini kilichopo Iringa akiwa amejikita zaidi katika fani ya IT (Informaion Technology) sanaa ya uigizaji alianza tangu akiwa shuleni chini ya usimamizi wa walimu pamoja na wazazi wake.

Aliingia rasmi kwenye sanaa ya uigizaji mnamo mwaka 2015 ambapo alijiunga na kikundi cha THT(Tanzania House Of Talent) akiwa kama mmoja wa wanakikundi hicho ambacho ndicho kilichokuwa mlango wake wa kupenya katika tasnia ya uigizaji na kumfanikisha kuigiza katika tamthiliya ya kelele sehemu ya kwanza.

 KELELE ni filamu ya kwanza kuigiza na ndiyo filamu ya pekee na yenye heshima kubwa sana kwake kwasababu ndiyo imemtambulisha katika sanaa ya uigizaji lakini pia imemuwezesha kujulikana zaidi na watanzania wengi.

Baadhi ya wasanii anaowakubali na anaopenda kazi zao kwa namna moja ama nyingine katika tasnia ya uigizaji ni pamoja na “Niva, Single Mtambalike,King Majuto pamoja na wengine wengi” hii ni kutokana na kuvutiwa sana na uigizaji wao na anapenda pia kufanyanao kazi katika tasnia hii ya uigizaji kama wasanii mwenzake.

“BIKO” mbali na sanaa anamiliki PIKIPIKI yake ambayo ameifanya kama sehemu ya ajira yani (bodaboda) ili aweze kujipatia kipato na kuweza kwa namna moja ama nyingine katika kujikimu na maisha yake ya kila siku.

                                         

                                        

            

 

 

 

Newsletter

Subscribe now to get Celebrity Exclusive Interview newsletter per month

Moview Everywhere

Visitors Counter

000281925
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
93
404
93
279557
8810
10020
281925

Your IP: 54.198.247.44
2017-09-25 03:45

Search