Emmanuel Mathias

Comedian
Share:

Personal Info

  • Birth Name: Emmanuel Mathias
  • Date of Birth: 01, Jan 1986
  • Residence: Dar es salaam
Social:

Biography

Emmanuel Mathias  almaarufu Mc pilipili alizaliwa mnamo mwaka 1986 katika wilaya ya Swaswa mkoani Dodoma,akiwa ni mtoto wa pili katika familia ya watoto watano.Kabila lake halisi ni Mgogo. 

Mnamo mwaka 1994 alianza elimu ya msingi katika shule K/ndege na kuhitimu katika shule ya msingi Ipagala, mwaka 2001 alijiunga katika shule ya Dodoma Sekondari kwa elimu ya Kidato cha Kwanza hadi cha Nne.Mnamo mwaka 2005 alifanikiwa kuendelea na  elimu yake katika shule ya Sekondari Distri Dubile kwa  kidato cha Tano na Sita. 

2007 alijiunga na chuo cha Ualimu cha Enkernford Tanga na kisha kuhitimu akiwa na taaluma ya Ualimu na kuanza kuifanyia  kazi taaluma yake kwa kufundisha shule mbalimbali ikiwemo shule ya Korogwe kilole Tanga.

Mc pilipili  alianza kukifahamu kipaji chake cha kuchekesha  akiwa na umri wa miaka 9.Alianza rasmi kukifanyia kazi kipaji chake pale alipofika kidato cha pili alianza rasmi shughuli za ushereheshaji (MC) katika sherehe mbalimbali za vijijini na hapo ndipo alipochanganya vichekesho pamoja na ushereheshaji. 

Miongoni mwa wasanii wa vichekesho waliomvutia sana kwa upande wake ni Trevor Noah, Basket mouth, (hawa wote ni wasanii wa bara la Afrika)  na kervin Hart ambaye ni Mmarekani .

Mpaka hivi sasa ameshafanya kazi pamoja na Eric Omondi (Kenya), Kansime (Uganda) ,Fred Omondi (Kenya) na Salvador (Uganda)

Baadhi ya kazi mbalimbali alizowahi  kufanya  katika stand up comedy Mc pilipili alifanya katika mikoa kama Dodoma, Geita, kahama, Arusha, Mbeya na Shinyanga Ikiwa ni moja ya malengo yake, bado Anaamini siku moja atasimama kama muasisi wa Sanaa  ya vichekesho vya jukwaani kwa Tanzania

Mbali na Sanaa ya vichekesho Mc pilipili pia ana taaluma ya ualimu ambayo ndiyo ameisomea, vilevile  ni mshehereshaji katika sherehe mbalimbali hiki pia ni kitu kikubwa anachokifanya  kwa sasa ukiondoa uchekeshaji.

 

Newsletter

Subscribe now to get Celebrity Exclusive Interview newsletter per month

Moview Everywhere

Visitors Counter

000300952
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
66
313
1582
297004
5309
11827
300952

Your IP: 54.224.18.114
2017-11-18 01:52

Search