Ndumbagwe Misayo

Director,Actress
Share:

Personal Info

  • Birth Name: Ndumbagwe Misayo
  • Date of Birth: 25, Dec 1992
  • Residence: Dar es salaam
Social:

Biography

Ndumbagwe Misayo almaharufu kama “THEA”,  alizaliwa mkoa wa Shinyanga akiwa ni mtoto wapili katika  familia ya mzee Ulasa, alihitimu elimu yake  ya msingi katika shule ya Mapambano na kuhitimu  elimu ya sekondari katika shule ya Green Victoria Academi.

 Akiwa kidato cha tatu alianza rasmi kujua kipaji chake kwa kuanza kuigiza maigizo ya shule,alijiunga na kikundi cha sanaa kilichokuwa na makazi yake eneo la kigogo, na alianza rasmi kucheza tamthiliya katika kituo c ha ITV katika kikundi cha MAMBO HAYO, alizidi kuvuka mipaka zaidi baada ya kuhamia katika kikundi kingine cha sanaa kilichojulikana kwa jina la KAOLE SANAA GROUP.

Baadhi ya filamu ambazo  ameshiriki na zimefanya vizuri katika soko la sanaa hapa nchini, ni pamoja na Why me, Dadas, Ukungu, Solemba, Segito, Tone la damu

Mbali na uigizaji  THEA ni mtayarishaji, muongozaji lakini pia ni mtunzi wa filamu za kibongo.

Malengo yake katika sanaa ni kufikisha mbali tasnia ya filamu ya bongo ili izidi kuvuka mipaka zaidi na kuzidi kuitambulisha tasnia ya filamu kimataifa, lakini pia anamalengo ya kufanya kazi na wasanii wakubwa  wa kimataifa kwasababu anaamini hii itamsaidia kujulikana zaidi pamoja na kuitangaza nchi ya TANZANIA.

Newsletter

Subscribe now to get Celebrity Exclusive Interview newsletter per month

Moview Everywhere

Visitors Counter

000300953
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
67
313
1583
297004
5310
11827
300953

Your IP: 54.224.18.114
2017-11-18 01:52

Search