Shiraz Ngassa

Upcoming Actor
Share:

Personal Info

  • Birth Name: Shiraz Ngassa
  • Date of Birth: 16, Mar 1992
  • Residence: Daresalaam
Social:

Biography

Shiraz Ngassa  alizaliwa mwaka 1992 katika hospitali ya Muhimbili, akiwa mtoto wa kwanza kati ya wa toto wanne upande wa baba yake.

Alianza elimu yake ya Msingi katika shule ya KIPAWA mnamo mwaka 1999 na kumaliza mwaka 2005, na kisha kwenda kujiunga na sekondari ya Al FAROUQ Boys mwaka 2006-2009 na kisha kuendelea na A level katika shule ya sekondari ya MZINGA mwa 2010-2012.

Kipaji chake cha uigizaji kilianza tangu akiwa darasa la nne kwa kujiunga katika kikundi kilichokuwa kinaitwa DHAHABU SANAA GROUP lakini mama yake alikuwa hataki aigize kwa kuhofia kuwa atakuwa na mahduhurio mabaya katika upande wa elimu.

Hakuwa na jinsi aliamua kuachana na uigizaji,lakini mungu alipomchukua mama yake na huku upande wa elimu Shirazi alikuwa kafika sekondari aliamua kuendelea na uigizaji na alipokuwa kidato cha pili alifanikiwa kuigiza filamu ya ‘TAMAA’ lakini haikutoka.

Alipomaliza kidato cha nne alijiunga na na kituo cha TINO MUYA FILM COMPANY na alifanikiwa kucheza filamu kama Gombero,Muuza uchafu,Mikono Salama ambayo alikuwa na Jb pamoja na Jokate lakini pia alicheza na tamthilia iliyokwenda kwa jina la ‘Kiza Kinene.’

Mwaka 2014 alitoka katika kikundi cha Tino na hapo ndipo yalipoibuka mashindano ya TANZANIA MOVIE TALENT (TMT) akaamua kushiriki na alifanikiwa kuwa mshindi wa pili ukanda,lakini hakufanikiwa kuingia fainali aliishia katika hatua ya nusu fainali lakini alifanikiwa tena kucheza filamu iliyokwenda kwa jina la mpango mbaya. 

Baada ya kuonekana katika mashindano hayo alifanikiwa kupata usimamizi kutoka katika kampuni ya SASENI MEDIA ambayo inamsimamia mpaka hivi.

Msanii anayemkubali katika filamu ni Michael Early amecheza filamu ya ‘The Perfect Guy’.

Newsletter

Subscribe now to get Celebrity Exclusive Interview newsletter per month

Moview Everywhere

Visitors Counter

000300951
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
65
313
1581
297004
5308
11827
300951

Your IP: 54.224.18.114
2017-11-18 01:52

Search