Single Mtambalike

Director,Script Writer,Actor
Share:

Personal Info

  • Birth Name: Single Mtambalike
  • Date of Birth: 05, Oct 1972
  • Residence: Dar-es-salaam
Social:

Biography

Single Mohamed Mtambalike almaarufu Kwa jina la ” Richie” alizaliwa mnamo tarehe 05,mwezi  10, mwaka 1972.

Mwaka 1980 alianza elimu ya Msingi katika shule ya  Mnazi Mmoja .Baada ya kuhitimu elimu yake ya Msingi ,mwaka 1987 aliendelea na elimu ya Kidato cha kwanza  katika shule ya Al-Haramain hadi mwaka 1990 alipohitimu kidato cha Nne.Baada ya kuhitimu vizuri masomo ya kidato cha Nne,mwaka 1991 alifanikiwa kuendelea na elimu ya Kidato cha Tano na Sita katika shule ya Sekondali ya Al-Haramain Islamic na kuhitimu kidato cha sita mwaka 1993.

Baada ya kuhitimu elimu ya Sekondari aliamua kujiunga na kozi  na mafunzo mbalimbali ikiwemo kozi ya Sanaa iliyokuwa ikitolewa na BASATA (Baraza la Sanaa Tanzania), kozi ya Uigizaji (UNICEF Training awareness art course iliyoendeshwa na ( TGNP).

Baada ya Kuhitimu kozi na mafunzo mbalimbali ya sanaa,mnamo mwaka 1997 alianza kuigiza katika  Tamthilia iliyojulikana kwa jina la MAMBO HAYO iliyokuwa ikionyeshwa na  kituo cha ITV. Mwaka 2000 aliendeleza fani yake kwa kuendelea kuigiza Tamthilia katika kituo cha CTN.Mwaka  2006 alijiunga na kampuni ya YERUSALEM FILM COMPANY  kama muigizaji na muongozaji.

Mbali ya Tamthilia alizocheza ” Richie” amecheza na kushiriki filamu mbalimbali,miongoni mwa filamu hizo ni pamoja na MAHABUBA, ONE & TWO,SWAHIBA,UYOGA,LELATO,SCENE YA BACHELOR,KITENDAWILI,MSALA,JESCA,THE QUEEN OF MASAI,SAFARI,MTAANI KWETU.

Miongoni mwa tuzo anayojivunia ni ushindi wa Tuzo ya AFRICA MAGIC VIWERS (2016) kwa kupitia filamu ya KITENDAWILI katika kipengere cha Filamu Bora ya Kiswahili.Mbali ya tuzo hiyo pia alikuwa Mshindi wa Tuzo ya MNET (2011 - 2012) katika kipengere cha Muigizaji Bora wa Kiume.

Tuzo nyingine alizowai kushiriki ni Tuzo ya EGOLI iliyofanyika nchini AFRIKA YA KUSINI na kushika nafasi ya Pili katika,na pia alishiriki katika Tuzo ya SHIWATA na kushinda katika kipengere cha Muigizaji Bora wa Kiume.

Mbali ya kuwa muigizaji na mwongozaji Single Mtambalike”Richie” ni miongoni mwa watu walioweza kuibua vipaji vya wasanii mbalimbali na baadae kuwa waigizaji na waongozaji  wakubwa ndani na nje ya nchi .Miongoni mwa matunda ya kazi ya uvumbuzi wa vipaji ni wasanii  kama JACOB STEVEN “JB”,VICENT KIGOSI “RAY”,R OSE NDAUKA, YVONE CHERY “MONALISA”, DIRECTOR JOHN KALAGE,HAJI ADAM,  DIRECTOR JOHN NA LISTER ambao hivi sasa ni waigizaji na waongozaji wakubwa   wa filamu.

 

Newsletter

Subscribe now to get Celebrity Exclusive Interview newsletter per month

Moview Everywhere

Visitors Counter

000300975
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
89
313
1605
297004
5332
11827
300975

Your IP: 54.224.18.114
2017-11-18 01:57

Search