Hemed Suleiman

Actor
Share:

Personal Info

  • Birth Name: Hemed Suleiman
  • Date of Birth: 05, Mar 1987
  • Residence: Dar-es-salaam
Social:

Biography

Hemed Suleiman almaarufu kama “PHD”  alizaliwa mnamo mwaka 1987 katika mkoa wa Tanga.Elimu yake ya msingi alianza kusoma katika shule ya Msingi KIPAWA  na kumalizia elimu yake katika shule ya msingi BUNGE.

Baada ya kuhitimu elimu yake ya msingi alifanikiwa kujiunga na shule ya Sekondari  ya ANNUR ISLAMIC kwa kidato cha Kwanza hadi cha Nne. Hemed Suleiman aliendelea na elimu yake ya kidato cha Tano na cha Sita katika shule ya Coastal High School ya Mkoani Tanga.

Muongozaji na Mtayarishaji George  Tyson ndiye alieona kipaji cha uigizaji cha Hemed kupitia mashindano ya TUSKER PROJECT FAME  ya mwaka 2009 baada ya kuona uwezo wake wa uchekeshaji na uigizaji .Baada ya kuisha kwa mashindano ya TUSKER PROJECT FAME  ndipo Muongozaji  George  Tyson alipoamua  kumshauri kuingia katika uigizaji wa  filamu .Alianza rasmi kuigiza katika filamu ya  WHO IS SMARTER  mwaka 2009 chini ya Mtaarishaji  na Muongozaji GEORGE TYSON.

Hemed Suleiman ameweza kucheza na kushilikishwa kwenye  filamu mbalimbali,miongoni mwa filamu alizocheza ni  KITORONDO ,CRAZY LOVE ,MY PRINCESS ,CONFUNSION,MKWE  na GUMZO

Hemed Suleiman ana ndoto ya kuja kuigiza filamu na MAJID msanii  kutoka nchini  Ghana na Denzel Washington kutoka Marekani. Mbali ya Sanaa ya uigizaji Hemed Suleiman pia anajihusisha na fani ya uimbaji wa mziki wa Bongo fleva.

 

 

Filmography

Latest Trailers And Videos

Newsletter

Subscribe now to get Celebrity Exclusive Interview newsletter per month

Moview Everywhere

Visitors Counter

000309203
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
364
301
665
306677
3954
9606
309203

Your IP: 107.20.120.65
2017-12-12 19:02

Search