Yvonne Cherryl

Actress
Share:

Personal Info

 • Birth Name: Yvonne Cherryl
 • Date of Birth: 19, Aug 1981
 • Residence: Dar-es-salaam
Social:

Biography

Yvonne Cherryl  kwa jina maarufu kama wengi walivyozoea kumuita “Monalisa” alizaliwa mnamo mwaka 1981 nchini Tanzania.

Yvonne Cherryl  amecheza na kushiriki filamu mbalimbali  kati ya Filamu ambazo hatoweza kuzisahau ni “Black Sunday”,filamu hii ilimpatia Tuzo ya Msanii Bora Tanzania mwaka 2010 kutoka  ZIFF,na Binti Nusa 2 & 3 filamu ya mwaka 2011 na kushinda Tuzo ya Central Award Best Actress in Tanzania.

 

Filamu nyingine alizocheza ni pamoja na “Payback”, “Nimeokoka”, “Cellular”, “Wrong Number”, “Wedding Pressure”, “Behind The Scene”, “Who is Smarter”, “Pastor Myambas Trial”, “Dilemma”, “Sabrina”, “38 Weeks”, “Girlfriend” na “Tell Me The Truth”.

 

She is My Sister ni filamu aliyoigiza na moja wa staa mkubwa kutoka nchini Nigeria “Nollywood”, Mercy Johnson chini ya mwogozaj (Director) Femi Ogedegbe.

 

Mbali ya Filamu Yvonne Cherryl  pia ameshiriki na kucheza michezo ya Jukwani kama ifuatayo

 1. A Man of The People at Kenya National Theatre (Nairobi, Kenya)
 2. Dont Dress For Dinner at Russian Cultural Centre (Tanzania)
 3. The Song of Lawino at Little Theatre (Tanzania)
 4. Zawadi ya Ushindi at ZIFF (Zanzibar)
 5. The Govt Inspector at Bagamoyo Art Festival
 6. Suoper Soul Sunday at National Museum of Tanzania

Yvonne Cherryl  katika sanaa ya uigizaji amefanikiwa kuchukua tuzo mbalimbali miongoni mwa tuzo hizo ni

 1. KIU Media,Queen of Bongo Films 2008
 2. Tuzo ya Msanii Bora Tanzania (2010) kupitia filamu ya “Black Sunday”
 3. Tuzo ya Central Award Best Actress in Tanzania (2011) kupitia filamu ya Binti Nusa 2 & 3
 4. Nigeria Entertainment Award, The Best Pan African Actress Nominee  

Mbali ya tuzo hizo Yvonne Cherryl  anajivunia tuzo ya Tanzania walk of Fame (2011) kama ni tuzo   muhimu sana kwenye maisha yake ya kisanaa yenye heshima  kubwa ya kuitangaza vizuri  nchi yetu kimataifa iliyoandaliwa na Global Publishers.

 

Mbali ya uigizaji wa filamu na michezo ya jukwaani Yvonne Cherryl  pia amehusika kwenye utengenezaji wa  matangazo mbalimbali ya kibiashara miongoni mwa matangazo hayo aliyoweza kushiriki ni

 1. Heineken (2001)
 2. Assas Diary Milk (2002)
 3. Comfy (2016)

Mbali ya Tuzo alizopata Yvonne Cherryl,kikubwa zaidi anachojivunia ni nafasi aliyopata ya kushiriki kwenye moja ya filamu iliyotayarishwa na watarishaji kutoka Hollywood inayoitwa Bleeding Sunshine ambayo imetayarishiwa nchini Ghana mwaka 2011 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Newsletter

Subscribe now to get Celebrity Exclusive Interview newsletter per month

Moview Everywhere

Visitors Counter

000300971
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
85
313
1601
297004
5328
11827
300971

Your IP: 54.224.18.114
2017-11-18 01:56

Search