×

Notice

Please enter your DISQUS subdomain in order to use the 'Disqus Comments (for Joomla)' plugin. If you don't have a DISQUS account, register for one here

Alichokisema Mh Nape Kuhusu Sera Ya Filamu

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema itaanza kukusanya maoni ya wadau wa filamu ili kuandaa sera itakayosaidia kutengeneza sheria mpya itakayosimamia tasnia hiyo kulingana na mazingira ya sasa.

Zoezi la ukusanyaji wa maoni litahusisha makundi mbalimbali wakiwemo watayarishaji, waigizaji na wasambazaji wa filamu.
Akizungumza kwenye kikao cha kujadili changamoto na mwelekeo wa tasnia hiyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam leo Jumanne, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema makundi yote yanapaswa kujitokeza kutoa maoni kulingana na changamoto wanazokabiliana nazo.

“Lazima tukubali wasanii mnatumia nguvu kubwa kufanya kazi lakini hamnufaiki, hamtakiwi kurudi nyuma. Tasnia hii ina sheria ya kipuuzi lazima tuanze mapema kujadiliana ili baadaye tutoke na mwongozo mzuri.”

source: Mwananchi

Rating:
( 1 Rating )

User Rating: 5 / 5

Star ActiveStar ActiveStar ActiveStar ActiveStar Active
 

Newsletter

Subscribe now to get Celebrity Exclusive Interview newsletter per month

Moview Everywhere

Visitors Counter

000300980
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
94
313
1610
297004
5337
11827
300980

Your IP: 54.224.18.114
2017-11-18 01:58