×

Notice

Please enter your DISQUS subdomain in order to use the 'Disqus Comments (for Joomla)' plugin. If you don't have a DISQUS account, register for one here

Heshima Na Maarifa Ni Chanzo Cha Mafanikio Lakini Sio Kwa BONGO MOVIE....

HABARI  za wakati  huu wapenzi wa filamu za Kitanzania  napenda niwakaribishe  kwenye makala hii fupi tuzungumze kwa  pamoja juu ya kuporomoka kwa soko la filamu na sanaa ya maigizo kwa ujumla.

Leo tuzungumzie chanzo au vyanzo vinavyopelekea wasanii wetu kutokupiga hatua kisanaaa na kuishia kuigiza katika filamu zenye ubora hafifu na zenye bajeti ndogo.

Mienendo na mabadiliko kitabia vinavyoonekana kuwa kikwazo nambari moja kupelekea soko la wasanii wetu kudorora nakuonekana wakawaida sana,tuchukulie mfano wa marehemu Stevean Kanumba enzi za uhai wake (mwenyezi Mungu ampunguzie adhabu ya kaburini) alikua ni masanii pekee aliyeonyesha uhai wa kuishi uhusika wake kama kioo cha jamii tofauti na wasanii wengine ambao wamekuwa  vioo vibovu hata kwa familia zao.

labda nitoe mfano hai nilio na ushahidi nao,  mwaka mmoja uliopita nilikua nakipindi cha Filamu za kitanzania  kilikuwa  kinaruka katika redio moja inaitwa chem chemi redio ipo huko Rukwa kilikua kipindi kizuri sana na kilikua na wasikilizaji wengi ambao wengi wao ndio wanunuzi wazuri wa kazi zetu tena DVD na sio zilizochakachuliwa kwani wengi wao bado wanatumia TV na Deki sio kompyuta .

kupitia kipindi cha filamu kwenye redio tulikua tunatangaza kazi zinazotarajia kuingia sokoni na hapa palikuwa patamu sana, nakumbuka  wakati movie ya mwalimu wangu Jimmy Mponda " J Plus"  ya Dable J final ilipokuwa inatarajia kutoka  nilipokea simu nyingi sana nikiulizwa inatoka lini mpka nikawa nashangaa hawa watu wanajua mimi ni msambazaji au, mbona simu nyingi kuuliza inatoka lini wengine wanauliza wataipataje  swala la kupokea simu nyingi nikaamini tunasikika kwa sehemu kubwa.

shida inakuja pale wasikiklizaji wanapoombaa kumsikia msanii wao  kwenye  maohojiano  (interview) ilinibidi nitafute mawasiliano kwa nguvu zote ili kuwapa wasikilizaji nini wanakihitaji,  juhudi zilizaa matunda kwa asilimia kubwa nilikua nafanikiwa kuwapata wahusika.

Swali ambalo mara nyingi lilikuwa linajirudia kwa Wasanii nilowaomba mahojiano lilikuwa  kituo gani kiko wapi na kinasikika dar es salaa,  mwingine alijitoa akili kabisa  eti  "mimi ni msanii mkubwa unajua sasa nikisikika kwenu ntakuwa nakipa kiki kituo hivyo mtanilipa bei gani"  hahahah  nacheka kama mazuri  wengine walijibu NIKO BUSY  sina muda  bila kuwasahau waliokubali  na ukifika muda wa mahojiano utapiga simu mpka ukome na akija kupokea jibu lake nipo kwenye pikipiki au la sivyo wasikilizaji wataambulia kusiki sauti ya mziki wa bar au milio ya pikipiki na magari huko barabarani.

nilipata bahati ya kuzungumza na  baadhi ya marafiki zangu wa vituo vikubwa vya habari nikitaka kujua kama hii hali ipo na kwao pia,majibu walonipa ni kuwa wasanii wengi  wapo radhi kutulipa garama tuende  kuwafanyia mahojiano kwa gharama yoyote.  Sasa nikawa najiuliza inamana watu wa media mikoani wanapataje taarifa zenu ili kuwafikishia ujumbe wanunuzi wa kazi zenu....?

Tabia ya dharau na kujiona nyinyi ndio ninyi muache mfikie hatua muwe na kikomo na heshima kwa watu wanao wazunguka pasipo kujali huyu anapesa au huyu ni nani katika jamiii.

Juzi juzi kulikuwa na majivuno ya baadhi ya wasanii waliokuwa na mikataba na kampuni fulani  ya usambazaji  walikuwa wakilala wakiamka wanapeleka makaratasi wanachukua mamilioni na mwisho wasiku wanatengeneza filamu zenye thamani na bajeti tofauti na pesa walizochukua wengine ikifika muda wakulipa kodi nyumba zao za kupanga au kuwapangisha wapenzi wao utasikia...

" chumba bei gani si milioni mbili (2) na kodi inahitajika mwezi ujao  basi subiri nifanye movie"  Bongo movie nini hiki imefikia hatua mnafanya movie ili kulipa madeni yenu na si kufanya movie kutengeneza soko lenu na kujikuza kiakili na kimaarifa tena  wenyewe mnaziitaga sinema................ tukutane chapter two (2)

 

Rating:
( 1 Rating )

User Rating: 5 / 5

Star ActiveStar ActiveStar ActiveStar ActiveStar Active
 

Newsletter

Subscribe now to get Celebrity Exclusive Interview newsletter per month

Moview Everywhere

Visitors Counter

000300958
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
72
313
1588
297004
5315
11827
300958

Your IP: 54.224.18.114
2017-11-18 01:53