×

Notice

Please enter your DISQUS subdomain in order to use the 'Disqus Comments (for Joomla)' plugin. If you don't have a DISQUS account, register for one here


Warning: in_array() expects parameter 2 to be array, null given in C:\Inetpub\vhosts\didasentertainment.com\httpdocs\plugins\content\spcomments\spcomments.php on line 70
Saturday, 24 September 2016 14:43

Jokate Amvutia Miss Njombe

Written by
Rate this item
(0 votes)

MREMBO Christina Mmbaga  aliyejinyakulia tuzo ya Miss Njombe na kushika nafasi ya sita katika Miss nyanda za Juu Kusini ambapo shindano hilo lilikuwa likishirikisha mikoa sita amefunguka na kudai kuwa aliyemfanya aingie katika tasnia hii ni Jokate Mwegelo.

Akizungumza na DidasEntertainment alisema kuwa licha ya kuwa alikuwa anapenda urembo toka zamani lakini mtu ambaye alikuwa akivutiwa nye katika tasnia hii ni mrembo Jokate Mwegelo ambaye alishiriki umiss,uigizaji na mwanamuziki.

"Nilikuwa napenda kiukweli umisi tangu nikiwa mdogo na nimefanya hivyo vizuri lakini kikubwa mtu ambaye nampenda na nina mvutia ni Jokate Mwegelo nimekuwa namfatilia na kuvutiwa naye hasa katika kazi zake na muonekano wake"alisema.

Akizungumzia kama ataendelea kuwepo katika fani hiyo ya umisi alisema kuwa ni ngumu tena kushiriki umisi huu kutokana na sheria kumbana lakini anaruhusiwa kufanya matangazo mbalimbali na kampuni zozote huku pia kwenda ngazi za juu na sio ngazi alizopitia.

"Katika ngazi hii ya umisi siruhusiwi tena kushiriki kutokana na sheria kunibana,lakini ninachoweza kufanya hivi sasa ni kufanya matangazo na kampuni mbalimbali alafu baadaye ni kushiriki umisi Tanzania kama mungu akipenda"alisema.

Christina alitoa wito kwa wasichana warembo kama yeye kuwa wasiwe waoga katika kufanya maamuzi ya kutaka kushiriki shindano lolote la kimisi na hata wazazi wasiwazuie kufanya kile kitu ambacho wanakipenda.

"Wanaopenda kufanya wasiwe waoga katika kufanya kile ambacho wanakipenda hii itafanya wawe na kujiamini kila muda katika maamuzi yao lakini pia wazazi wasiwabane watoto wao"alisema mrembo huyo anayetumia vipodozi vya kampuni ya Mac. 

Read 429 times Last modified on Thursday, 29 September 2016 16:15

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.

Newsletter

Subscribe now to get Celebrity Exclusive Interview newsletter per month

Moview Everywhere

Visitors Counter

000300968
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
82
313
1598
297004
5325
11827
300968

Your IP: 54.224.18.114
2017-11-18 01:56