×

Notice

Please enter your DISQUS subdomain in order to use the 'Disqus Comments (for Joomla)' plugin. If you don't have a DISQUS account, register for one here


Warning: in_array() expects parameter 2 to be array, null given in C:\Inetpub\vhosts\didasentertainment.com\httpdocs\plugins\content\spcomments\spcomments.php on line 70
Saturday, 24 September 2016 13:57

BIKO “Nidhamu Ni Siri Ya Mafanikio”

Written by
Rate this item
(0 votes)

Msanii anayekuja kwa kasi katika tasnia ya uigizaji nchini Mangasini Scanda almaarufu BIKO amewasihi wasanii wenzake wanaochipukia katika sanaa ya uigizaji kuwa na nidhamu bora katika kazi zao ili kujitengenezea nafasi nzuri kwa wasanii wakongwe katika kupata fursa nzuri ya kushirikishwa katika kazi mbalimbali za wasanii  hao.

Akizungumza na Didasentertainment mapema leo amesema wanasanii wakonge wanawachukulia wasanii chipukizi kama wasanii wa ziada kutokana na kukosa nidhabu ya kutosha, japokuwa wanavipaji vizuri na vyakutosha katika sanaa ya uigizaji na ndiyo maana wanawahitaji pindi tu pale wanapoona kuna nafasi ya mtu imepelea na isiyokuwa ya muhimu sana na kuamua kutafuta msaanii anayechipukia na kumuweka.

“Kwakweli sababu inayosababisha wasanii wakongwe kushindwa kutojihusisha ama kuwashirikisha wasanii wanaochipukia ni kutokana na kutokuwa na nidhamu ya kutosha miongoni mwao hivyo wasanii wakongwe kushindwa kuwa na imani ya kutosha miongoni mwa wasanii hao wanaochipukia katika tasnia hii ya uizaji”. Alisema Biko

Lakini pia amewataka wasanii wanaochipukia kujiamini wao wenyewe na kujiwekea misingi imara katika kazi zao ili kupata fursa za pekee, bila kusahau kuwa na nidhamu ya kutosha ambayo ndiyo funguo bora ya maendeleo ya kazi yoyote na kazi ambazo ziko nje ya sanaa.

“Wasanii wachanga na wale tunaochipukia tuwe na nidhamu ya kutosha kwani hii ndiyo nguzo imara ambayo itatupa fursa nzuri katika kazi zetu za sanaa na zitatuwezesha kufika mbali zaidi na kuweza kutambulisha kazi zetu za sanaa nje na ndani ya nchi yetu”. Aliongeza Biko

Hatahivyo amebainisha baadhi ya wasanii anaowakubali na anaopenda kazi zao kwa namna moja ama nyingine katika tasnia ya uigizaji ni pamoja na Niva, Single Mtambalike, King Majuto pamoja na wengine wengi, hii ni kutokana na kuvutiwa sana na uigizaji wao na anapenda pia kufanya nao kazi katika tasnia hii ya uigizaji kama wasanii wenzake.

Read 415 times Last modified on Saturday, 24 September 2016 14:20
More in this category: Wasanii Wachanga Tusijishushe »

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.

Newsletter

Subscribe now to get Celebrity Exclusive Interview newsletter per month

Moview Everywhere

Visitors Counter

000300974
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
88
313
1604
297004
5331
11827
300974

Your IP: 54.224.18.114
2017-11-18 01:57